Jamhuri ya Watu wa Zanzibar
From Wikipedia
Lugha ya Taifa | Kiswahili | ||
Mji Mkuu | Zanzibar | ||
Rais | Amani Abeid Karume | ||
Eneo | 121,320 km² |
||
Wakazi | 984,625 |
||
Dini | Waislamu takriban 96-99%, Wakristo, Wahindu | ||
Uhuru | Kutoka Uingereza 19.12.1963, Mapinduzi 12.01.1964 |
||
Fedha | TSh |
Jamhuri ya Watu wa Zanzibar ni sehemu ya Jamhuri ya Maungano ya Tanzania inayojitawala katika mambo yake ya ndani. Eneo lake ni sawa na funguvisiwa ya Zanzibar iliyopo mbele ya mwambao wa Afrika ya Mashariki karibu na Tanganyika au Tanzania bara. Inajumuisha visiwa vikubwa vya Unguja na Pemba pamoja na visiwa vidogovidogo. Kwa jumla mikoa mitano ya Tanzania imo ndani ya Zanzibar ikiwa mitatu iko Unguja na miwili Pemba.
Zanzibar inatawaliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ). Raisi Amani Abeid Karume aliyekuwa mgombea wa CCM amechaguliwa mara ya pili na wananchi wote tar. 30.10. 2005 katika kura iliyopingwa na chama cha Upinzani CUF.
Zanzibar ina Bunge lake lenye wabunge 50 wanaochaguliwa kwa muda wa miaka mitano.
Mji mkuu na makao makuu ya serikali ni Jiji la Zanzibar ambalo liko kisiwa cha Unguja. Mji mkuu wa kisiwa cha Pemba ni Chake Chake. Idadi ya wakazi wote ilikuwa 984,625 mwaka 2002, wakiwa 622.459 wakazi wa Unguja na 362.168 wakazi wa Pemba.
Biashara ya Zanzibar ni kilimo na utalii. Mazao yanayouzwa nje ni hasa karafuu, basibasi, mdalasini na pilipili.
[edit] Viuongo vya nje
- Tovuti ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar
- (en)Takwimu
- (fr)Picha za Zanzibar
- (en)Ramani ya Zanzibar na Tanganyika 1886
- (en)Makala ya BBC kuhusu bendera mpya
- Historia na utamaduni wa Zanzibar
- (en)Zanzibar links
|
|
---|---|
Arusha | Dar es Salaam | Dodoma | Iringa | Kagera | Kigoma | Kilimanjaro | Lindi | Manyara | Mara | Mbeya | Morogoro | Mtwara | Mwanza | Pemba Kaskazini | Pemba Kusini | Pwani | Rukwa | Ruvuma | Shinyanga | Singida | Tabora | Tanga | Unguja Kaskazini | Unguja Kusini | Unguja Mjini Magharibi | |
Categories: Tanzania | Zanzibar | Mbegu