Karne ya 7
From Wikipedia
Karne ya 7 ilikuwa kipindi cha miaka mia moja kati ya 601 hadi 700. Kikamilifu kilianza tar. 1 Januari 601 na kuishia 31 Desemba 700. Namba zake zinafuata hesabu ya miaka "baada ya Kristo".
Kama kila "karne" ni kipindi kinachohesabiwa kwa hiari ya kibinadamu kwa sababu ni mgawanyo wa kalenda tu - hali halisi maendeleo na mabadiliko makubwa hayafuati migawanyo ya kalenda ya kibinadamu.
Kuna mambo mengi yaliyotokea wakati wa karne hii.
[edit] Karne ya Waarabu
- Dini mpya ya Uislamu inaanza Uarabuni
- Waarabu watoka katika Bara Arabu na kuvamia milki za jirani za Bizanti na Uajemi zilizowahi kuchoshana kwa vita ndefu
- Hadi mwisho wa karne jeshi za Waarabu Waislamu zafika kwenye milango ya Ulaya, China na Uhindi na kutawala maeneo makubwa yote kuanzia Afrika ya Kaskazini hadi Asia ya Kati.