Kiafrikaans
From Wikipedia
Kiafrikaans (Afrikaans) ni lugha ya Afrika Kusini iliyotokea katika karne nne zilizopita kwenye msingi wa Kiholanzi pamoja na athari za lugha mbalimbali. Imekuwa lugha rasmi katika Afrika Kusini tangu mwaka 1925 badala ya Kiholanzi. Hata kama ni lugha iliyozaliwa Afrika kitaalamu ni kati ya lugha za Kigermanik.
Kiafrikaans ina wasemaji wa lugha ya kwanza milioni sita na milioni kumi wasemaji kama lugha ya pili.
Kiasili kimetokea kama lugha ya makaburu ya Afrika Kusini lakini imekuwa pia lugha ya wakazi chotara katika jimbo la Rasi Magharibi ("Cape Coloureds"). Leo hii wasemaji wa asili ya Ulaya ni chini ya nusu ya wasemaji wote wa Kiafrikaans.
Ni lugha rasmi mojawapo Afrika Kusini pamoja na lugha 9 nyingine. Ni pia kati ya lugha ya kitaifa huko Namibia.