Kibelarus
From Wikipedia
Kibelarus (Беларуская мова, "biełaruskaja mova" - lugha ya Kibelarus) ni lugha ya watu wa Belarus ikiwa ni moja kati ya lugha tatu za Kislavoni cha Mashariki pamoja na Kiukraine na Kirusi. Kibelarus inashirikiana maneno ya lugha hizi pia imepokea sehemu ya msamiati wake kutoka Kipoland kutokana na historia ndefu ya pamoja kati ya Poland na Belarus. Lugha za Kislavoni ni sehemu ya jamii ya Lugha za Kihindi-Kiulaya.
Kibelarus huandikwa mara nyingi kwa mwandiko wa Kikyrili lakini kuna pia namna ya kuiandika kwa mwandiko wa Kilatini.
Idadi ya wasemaji ni kati ya milioni 7 au 8. Kibelarus ni lugha rasmi katika nchi ya Belarus. Kuna pia wasemaji Poland katika eneo la Białystok) halafu kati ya vikundi vya wahamiaji waliotoka Belorus na kukaa Marekani, Kanada au Australia.