Kuomintang
From Wikipedia
Kuomintang ni chama cha kisiasa katika Jamhuri ya China.
Iliundwa mwaka 1919 na Sun Yat-sen kama chama cha Jamhuri ya China. Mfuasi wake kama kiongozi wa chama alikuwa Chiang Kai-shek. Kuomintang ilitawala China hadi 1949 iliposhindwa na Wakomunisti chini ya Mao Zedong katika vita ya wenyewe kwa wenyewe ya China. Wafuasi wengi walihamia kisiwa cha Taiwan na kuendeleza chama chao huku.
Kuomintang ilikuwa chama cha pekee cha Taiwan (Jamhuri ya China) kilichoruhusiwa hadi 1991. Tangu mwaka 2000 Kuomintang imeshindwa katika uchaguzi imekuwa chama cha upinzani.
Categories: Mbegu | Uchina | Taiwan