Orinoco
From Wikipedia
Mto wa Orinoco | |
---|---|
|
|
Chanzo | Milima ya Parima mpakani wa Venezuela na Brazil |
Mdomo | Bahari ya Karibi (Atlantiki) Mdomo wa pili: kupitia mto wa Amazonas |
Nchi za beseni ya mto | Venezuela, Kolombia |
Urefu | 2,140 km |
Kimo cha chanzo | 1,047 m |
Kiasi cha maji kinachotolewa mdomoni | 33,000 m³/s kwa wastani |
Eneo la beseni (km²) | 953 600 km² |
Mto Orinoco ni kati ya mito mikubwa kabisa ya Amerika ya Kusini mwenye urefu wa 2,410 km.
Ni mto wa pekee kwa sababu una midomo miwili tofauti: njia kuu ya maji huelekea kwenye delta ya mto katika bahari ya Karibi. Lakini mkono mmoja unafikisha sehemu ya maji yake katika mto wa Amazonas.
Delta ya Orinoco ilikuwa mahali ambako Kristoforo Kolumbus alikanyaga mara ya kwanza bara la Amerika mwaka 1498.