Richard Feynman
From Wikipedia
Richard Phillips Feynman (11 Mei, 1918 – 15 Februari, 1988) alikuwa mwanafizikia kutoka nchi ya Marekani. Anaangaliwa kuwa mwanafizikia mashuhuri kabisa baada ya Vita Kuu ya Pili ya Dunia. Hasa aliendeleza nadharia ya nuru, yaani nuru ielezwe kama yote mawili wimbi na chembe. Mwaka wa 1965, pamoja na Julian Schwinger na Shinichiro Tomonaga alikuwa mshindi wa Tuzo ya Nobel ya Fizikia.