Yuri Gagarin
From Wikipedia
Yuri Alexeyevich Gagarin (Kirusi Юрий Алексеевич Гагарин), alizaliwa tarehe 9 Machi, 1934 huko Klushino karibu na Smolensk, Urusi; alifariki tarehe 27 Machi, 1968. Alikuwa mwanadamu wa kwanza aliyefika angani.
Alimwoa Valentina Goryachova akawa na mabinti wawili naye. Akajiunga na Jeshi la Anga la Urusi mwaka 1955.
Mwaka 1960 aliteuliwa katika kikosi cha kwanza cha marubani walioandaliwa kurushwa kwa anga la nje akateuliwa kuwa mtu wa kwanza wa kutoka duniani.
Tarehe 12 Aprili, 1961 alirushwa na chombo cha angani Vostok 1 akizunguka dunia lote mara moja katika muda wa dakika 108. Akashuka Siberia.
Alipandishwa cheo na kuwa mkuu wa kituo cha kuandaa wanaanga Warusi. Mwaka 1968 alikufa katika ajali ya ndege alipofanya mazoezi ya urubani akazikwa kwenye makaburi ya heshima huko Moscow.