Zama za Kati
From Wikipedia
Zama za Kati zilihusisha wakati wa katikati katika mgawanyo wa kitamaduni wa historia ya Ulaya katika “zama” tatu: ustaarabu wa
- Zama za Kale,
- Zama za Kati, na
- Wakati wa Kisasa.
Kwa kawaida, Zama za Kati za Ulaya Magharibi huhesabiwa toka mwisho wa Dola la Roma ya Magharibi (karne ya 5) hadi kuanza kwa falme za kitaifa, mwanzo wa uvumbuzi wa ng’ambo ya Ulaya, Mwamko wa Kipagani, na Matengenezo ya Waprotestanti kuanzia mwaka 1517. Mabadiliko haya yalionesha mwanzo wa kipindi cha Zama za Kisasa ambacho kilitangulia mapinduzi ya viwanda.
Zama za Kati hujulikana kama “Kipindi cha Mediavo”, au kifupi “mediavo” (mara nyingine hutamkwa mediaevo au kihistoria, medievo).