Alfabeti ya Kilatini
From Wikipedia
Alfabeti ya Kilatini inayotumiwa kwa lugha nyingi duniani. Hata Kiswahili huandikwa siku hizi kwa herufi za Kilatini kama kwa mfano ukurasa huu wa wikipedia.
Contents |
[edit] Mwanzo wa alfabeti ya Kilatini
Asili ni namna ya kuandikwa kwa lugha ya Kilatini iliyokuwa lugha ya Roma ya Kale. Baadaye ilitumiwa kuandika hata lugha za Kirumi, Kigermanik, Kislavoni, Kituruki na pia lugha za Afrika na za Kiasia.
Waroma walipokea alfabeti yao kutoka alfabeti ya Kigiriki lakini waliibadilisha hasa kwa kuacha kando herufi za kutaja sauti ambazo hazikuwa na maana katika Kilatini.
Alfabeti ya kwanza ya Kilatini ilikuwa na herufi 21 pekee:
- A B C D E F Z H I K L M N O P Q R S T V X
Baada ya kuvamia Ugiriki Waroma wa Kale walianza kutumia maneno mengi ya Kigiriki katika lugha yao hivyo wakaingiza herufi mbili za ziada kutoka Kigiriki kwa ajili maneno haya mapya ni Y na Z.
[edit] Namna ya kuandika
Waroma wa Kale waliandika herufi kubwa tu. Tena hawakuacha nafasi kati ya maneno hivyo maandiko yao si rahisi ya kusoma:
Mfano wa maandishi ya Kiroma:
- AVREAPRIMASATAESTAETASQVAEVINDICENVLLO
- SPONTESVASINELEGEFIDEMRECTVMQVECOLEBAT
Siku hizi inaandikwa hivyo:
- Aurea prima sata est aetas, quae vindice nullo,
- sponte sua, sine lege fidem rectumque colebat.
[edit] Nyongeza za baadaye
Baada ya mwisho wa Dola la ROma ni hasa mataifa ya Ulaya yaliyotumia alfabeti ya Kilatini. Wakati wa karne za kati herufi zifuatazo ziliongezwa kufuatana na mahitaji ya lugha za Waulaya:
- herufi za I na V zilimaanisha konsonanti na pia vokali. Hapa herufi mpya za "J" na "U" ziliingizwa.
- herufi ya W ilitokea baada ya kuandika VV mwanzoni
Hivyo Alfabeti inayojulikana leo hii kama "kilatini" imepatikana hivyo:
-
- A, B, C, D, E, F, G, H, I, J, K, L, M, N, O, P, Q, R, S, T, U, V, W, X, Y, Z.
- a, b, c, d, e, f, g, h, i, j, k, l, m, n, o, p, q, r, s, t, u, v, w, x, y, z.
[edit] Herufi za nyongeza katika lugha mbalimbali
Kwa mahitaji ya lugha mablimbali kuna nyongeza nyingi katika alfabeti ya Kilatini (mifano):
-
-
- herufi za ä, ö, ü zinatumiwa katika Kijerumani, Kituruki na Kifinland
- herufi kama ã au ñ (Kireno)
- herufi kama ž, č, š (lugha za Kislavoni)
- herufi kama ng' (Kiswahili)
-
Hii ni mifano michache tu.
[edit] Uenezaji wa alfabeti ya Kilatini
Uwezo wa kupokea alama mpya ni sababu ya uenezaji wa alfabeti ya Kilatini. Kuna lugha mbalimbali zolizowahi kuandikwa kwa alfabeti tofauti lakini zilipokea ile ya Kilatini. Hata kama sababu muhimu ilikuwa utawala wa kikoloni katika sehemu nyingi za dunia kuna pia faida zilizosababisha kuendelea na alfabeti ya Kilatini hata baada ya kupata uhuru.
Mfano ni lugha kama Kiswahili na Kituruki zilizowahi kuandikwa kwa mwandiko wa Kiarabu.
Kiswahili kilianza kuandikwa na Wazungu kama Krapf kwa herufi za Kilatini katika karne ya 19. Katika karne ya 20 Waingereza walisanifisha lugha kwa kutumia alfabeti ya Kilatini. Faida yake ni ya kwamba sauti nyingi zinatajwa vizuri zaidi kuliko kwa Kiarabu.
Kituruki kilianza kutumia herufi za Kilatini baada ya mapinduzi ya Atatürk.
Hata Uchina