Bremen
From Wikipedia
Bremen ni mji mwenye bandari muhimu katika Ujerumani ya Kaskazini. Iko kando ya mto Weser takriban 50 km kabla haujaingia katika Bahari ya Kaskazini. Ina wakazi 546,000. Pamoja na eneo la jirani kuna watu milioni 2.37 katika mazingira ya Bremen. Weser inapanuka baada ya kupita mji kuwa na mdomo pana sana kabla ya kuishia baharini hivyo meli zinaweza kufika hadi mjini.
Bremen ni dola-mji ikiwa ni moja ya majimbo 17 ya kujitawala ya Ujerumani. Jina rasmi ni „Mji huru wa Hanse wa Bremen“ (Freie Hansestadt Bremen). Hanse ilikuwa shirikisho la kimataifa la miji ya biashara iliyojitawala zamani za nyakati za kati. Kwa muda mrefu wa historia yake Bremen ilikuwa kama nchi ndogo ya kujitegema hadi kujiunga na Dola la Ujerumani 1871. Jimbo la Bremen ina miji miwili ya Bremen yenyewe na Bremerhaven.
Wafanyabiashara wa Bremen waliwahi kuwa na biashara na nchi za nje kwa jahazi na meli zao tangu karne nyingi. Hata mawasiliano kati ya Afrika na Ujerumani yalipitia hasa Bremen na mji jirani wa Hamburg.