Jonas Savimbi
From Wikipedia
Jonas Malheiro Savimbi alikuwa ni kiongozi wa vita vya msituni nchini Angola. Savimbi alizaliwa 3 Agosti 1934 na kufariki 22 Februari 2002. Mwaka 1966 alianzisha vuguvugu la UNITA (kireno: União Nacional para a Independência Total de Angola) kama harakati ya kukomboa Angola kutoka ukoloni wa Ureno.
UNITA ilikuwa moja kati ya harakati tatu zilizoshindana. UNITA ilianza kama kikundi chenye itikadi ya kikomunisti kufuatana na itikadi ya Mao Zedong. Uadui kati ya wakomunisti wa Uchina na Urusi ulionekana katika mashindano ya UNITA dhidi ya MPLA iliyosaidiwa na Urusi. Baada ya uhuru mwaka 1975 MPLA ilitawala mji mkuu na serikali rasmi lakini Savimbi aliendelea kuipinga.
Savimbi alipata a kupokea baadaye usaidizi kutoka maadui wote wa MPLA bila kujali itikadi. UNITA ilipata misaada toka serikali mbalimbali duniani ili kuiondoa madarakani serikali ya MPLA (kireno: Movimento Popular de Libertação de Angola - Partido do Trabalho).
Savimbi alikuwa akipata misaada ya fedha na silaha toka serikali za Marekani, China, Afrika Kusini, Ivory Coast, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (wakati huo ikijulikana kama Zaire), Moroko, n.k. Serikali ya Angola ilikuwa ikipata misaada toka Urusi, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kijerumani, Kuba, na Nicaragua.
Savimbi aliuawa vitani 22 Februari 2002.
[edit] Viungo vya nje
- Tamko la Ikulu ya Marekani kuhusu mkutano kati ya rais wa Marekani na Jonas Savimbi, June 30, 1988".
- "The Coming Winds of Democracy in Angola" - Hotuba ya Jonas Savimbi nchini Marekani, Oktoba 5, 1989
- Habari ya BBC kuhusu kifo cha Savimbi,
- Tamko la serikali ya Angola kuhusu kifo cha Jonas Savimbi