Martin Luther
From Wikipedia
Martin Luther (10 Novemba, 1483 – 18 Februari, 1546) alikuwa mwanateolojia kutoka nchi ya Ujerumani. Alijiunga na kituo cha watawa, aliwekwa wakfu kama padre na kuwa profesa kwenye chuo kikuu cha Wittenberg. Swali lililomtesa kwa muda mrefu, yaani "Vipi nipate Mungu mwenye huruma?", limejibiwa aliposoma Barua kwa Waroma, sura ya 3, mstari wa 24: "kwa zawadi ya neema ya Mungu, watu wote hukubaliwa kuwa waadilifu kwa njia ya Yesu Kristo anayewakomboa." Luther alianza kupinga bidii zote za kanisa za kuwakomboa watu kupitia matendo au sadaka zao (madekezo). Tarehe 31 Oktoba, 1517, alitolea "Hoja 95 dhidi ya madekezo" (kwa Kijerumani: 95 Thesen wider den Ablass) kimaandishi. Hii ilimsababisha kugombana hata na Papa wa Roma, na kutengwa na kanisa akiongoza Mageuzo ya Kanisa. Aliandika vitabu vingi, kutunga nyimbo kadhaa na kutafsiri Biblia katika lugha ya Kijerumani.