Mwaka wa nuru
From Wikipedia
Mwaka wa nuru ni kipimo si cha muda lakini cha umbali. Kinataja umbali unaopitiwa na nuru ikitembea kwa muda wa mwaka moja ya dunia yaani siku 365.
Msingi wa kipimo hiki ni kasi ya nuru ya kuwa nuru inatembea takriban kilomita 300,000 kwa sekunde. Idadi kamili ni mita 299,792,458 kwa sekunde moja. Mwezi wa dunia yetu una umbali na sisi kama sekunde moja wa nuru au kilomita lakhi tatu na dunia.
Katika mwaka moja umbali huo unafika mita 9.461 × 1015.
Kipimo hiki kinahitajika kutaja umbali kati ya nyota na nyota angani. Umbali huu umepimwa kuwa miaka ya nuru mamia, maelfu au hata mamilioni. Kutokana na ukubwa wa ulimwengu umbali katika anga ni kubwa sana. Nyota jirani kabisa na jua letu inaitwa Alpha Centauri umbali wake ni 4.2 miaka ya nuru maana yake nuru yake inahitaji zaidi ya miaka minne hadi imefika kwetu. Kwa maana nyingine tunaiona nyota hii jinsi ilivyoonekana miaka minne iliyopita.