Rungwe (wilaya)
From Wikipedia
Wilaya ya Rungwe ni kati ya wilaya 8 za Mkoa wa Mbeya katika Tanzania. Imepakana na Wilaya ya Mbeya vijijini upande wa kaskazini, Mkoa wa Iringa upande wa mashariki, Wilaya ya Kyela upande wa kusini-mashariki, Wilaya ya Ileje kwa kusini-magharibi na Mbeya mjini kwa magharibi. Makao makuu ya wilaya yako Tukuyu.
Mwaka 2002 wilaya ilikuwa na wakazi 307,270.[1] Rungwe ni hasa eneo la Wanyakyusa ikishika sehemu kubwa ya eneo la Unyakyusa. Jina la wilaya limetokana na kituo cha misioni ya Moravian cha Rungwe kilichopo kwenye mitelemko ya mlima wa Rungwe takriban 20 km kutoka Tukuyu.
Kati ya mazao ya sokoni kuna mashamba makubwa ya chai. Rungwe inapokea mvua nyingi iko kati ya maeneo yenye rutba sana katika Tanzania.
Barabara kuu kutoka Daressalaam - Iringa - Mbeya kwenda Malawi inapita eneo la wilaya.
[edit] Tarafa
Wilaya ya Rungwe ina tarafa 30:
|
|
|