Wikipedia
From Wikipedia
Wikipedia ni kamusi elezo huru ya lugha nyingi katika mtandao. Inatumia taratibu wa wikiwiki. Ni bure kabisa, na inaweza kusomwa, kuandikwa, na kuhaririwa na mtu yeyote, popote pale. Yaani kila mtu anaweza kuchangia makala au kuwa na uhuru wa kuboresha makala zilizopo kwa kuzihariri.
Kamusi hii inajengwa kwa utaratibu huria ambao umejengwa juu ya falsafa ya ushirikiano inayokuwa kwa kasi. Falsafa hii inaonekana katika vuguvugu la programu huria ya tarakilishi, mikutano huria, demokrasia huria, n.k.
[edit] Historia
Wikipedia ilianzishwa kwa Kiingereza mwezi wa kwanza mwaka 2001. Mwaka 2003 kamusi elezo hii ilianzishwa katika lugha ya Kiswahili.