Ghuba ya Uajemi
From Wikipedia
Ghuba ya Uajemi (Kiajemi: خلیج فارس khalij-e fārs; Kiarabu: الخليج الفارسي al-khalīj al-fārsī; pia: الخليج العربي al-khalīj al-ʿarabī „Ghuba Arabu“; zamani pia "Ghuba ya Basra" - hadi leo kituruki Basra Körfezi) ni ghuba kubwa la Bahari Hindi kati ya Uajemi na rasi ya Uarabuni.
Ni kawaida ya kuiita ghuba ya Uajemi lakini katika fitina ya miaka iliyopita nchi kadhaa za Waarabu ziliita "Ghuba Arabu".
[edit] Nchi jirani
Nchi zinazopakana na ghuba ni:
[edit] Umuhimu wa kisiasa na kiuchumi
Nchi za ghuba zimekuwa muhimi sana duniani kwa sababu ya mafuta ya petroli inayopatikana hapa kwa wingi. Utajiri huu umebadilisha uso wa nchi zinazopakana na ghuba.
Utajiri huo umesababisha pia vita kadhaa kama vile vita ya Iran-Iraq, vita ya Iraq-Kuwait, vita ya ghuba.
[edit] Jiografia
Eneo lote la ghuba ni 233,000 km². Maji matamu huingia kwa njia ya mito ya Frati na Hidekeli inayoungana katika Shat al-Arab.
Urefu wake ni takriban 1,000 km na upana wake kati ya 200 hadi 300 km. Kina hakizidi 100 m.
Mlango wa Hormuz unaunganisha ghuba na Bahari Arabu ambayo ni bahari ya kando ya Bahari Hindi.