Kisiwa
From Wikipedia
Kisiwa ni eneo la nchi kavu ndani ya bahari, ziwa au mto linalozungukwa na maji wakati wote. Ukubwa wake hautoshi kuitwa "bara".
Visiwa vilivyoko karibu kama kundi mara nyingi huitwa "funguvisiwa".
Tofauti kati ya kisiwa kikubwa na bara dogo limeamuliwa kati ya
- Greenland inayoitwa kisiwa kikubwa duniani chenye eneo la kilomita za mraba milioni 2.1 na
- Australia inayotazamiwa kuwa bara dogo duniani lenye eneo la kilomita za mraba milioni 7.7.