Chad
From Wikipedia
|
|||
Hadabu ya Taifa: Unité - Travail - Progrès | |||
Lugha za Taifa | Kifaransa, Kiarabu | ||
Mji Mkuu | Ndjamena | ||
Rais | Idriss Déby | ||
Fedha | Franc CFA | ||
Saa za Eneo | UTC +1 | ||
Wimbo wa Taifa | La Tchadienne | ||
Intaneti TLD | .td | ||
Codi ya simu | 235 |
Chad (pia: Chadi) ni nchi iliyoko Afrika ya Kati. Mji mkuu ni Ndjamena. Imepakana na Libya, Sudan, Jamhuri ya Afrika ya Kati, Kamerun, Nigeria na Niger.
[edit] Jiografia
Sehemu kubwa ya eneo lake ni jangwa na nchi yabisi. Katika kusini kuna kanda lenye hali ya hewa ya kitropiki lakini ardhi yenye rutba inayofaa kwa kilimo ni asilimia 3 za aeno lote tu.
Katika kaskazini kuna milima ya Tibesti. Katikati iko beseni ya ziwa Chad lililokuwa kati ya maziwa makubwa kabisa duniani lakini limekonda sana katika miaka iliyopita.
[edit] Watu
Jinsi ilivyo katika nchi mbalimbali za kanda la Sahel kuna aina mbili za wakazi ndani yake:
- Kaskazini wako hasa watu walioathiriwa sana na utamaduni wa Kiislamu. Mifano ni Waarabu, Wafulbe, Wahaussa, Wazaghawa na wengine. Wengi wao walikuwa wafugaji na sehemu ya makabila inaendelea hadi leo maisha ya kuhamahama.
- Kusini wako hasa watu wanaofuata dini za jadi za Kiafrika au Ukristo kama Wasara. Wengi wao hulima.
Katika historia kabla ya ukoloni watu wa kaskazini waliwafanyia vita watu wa kusini na kuteka wafungwa kama watumwa. Hadi leo uhusiano kati ya kusini na kaskazini ya nchi ni mgumu.
[edit] Historia
Makala hiyo kuhusu "Chad" bado ni mbegu. Unaweza kusaidia kuikuza kwa kubofya kitufe kilichoandikwa "hariri". Ikiwepo makala kuhusu Chad kwa lugha nyingine, unaweza kuitafsiri kwa Kiswahili. |
Makala hiyo kuhusu "Chad" ni fupi mno. Inahitaji kupanushwa karibuni. |
Nchi za Afrika | |
---|---|
Afrika ya Kati (Jamhuri ya) | Afrika Kusini | Algeria | Angola | Benin | Botswana | Burkina Faso | Burundi | Cabo Verde | Chad |Cote d'Ivoire | Djibouti | Eritrea | Gabon | Gambia | Ghana | Guinea | Guinea Bisau | Guinea ya Ikweta | Kamerun | Kenya | Komori | Kongo (Jamhuri ya) | Kongo (Jamhuri ya Kidemokrasia ya) | Lesoto | Liberia | Libya | Madagaska | Malawi | Mali | Misri | Morisi (Visiwa vya) | Mauritania | Moroko | Msumbiji | Namibia | Niger | Nigeria | Rwanda | Sahara ya Magharibi | Sao Tome na Principe | Senegal | Shelisheli | Sierra Leone | Somalia | Sudan | Tanzania | Togo | Tunisia | Uganda | Uhabeshi | Uswazi | Zambia | Zimbabwe | |
Maeneo ya kiafrika ambayo ni sehemu za nchi nje ya Afrika | |
Ufaransa: Mayotte · Réunion | Hispania: Visiwa vya Kanari · Ceuta · Melilla | Ureno: Visiwa vya Madeira | Uingereza: · Kisiwa cha St. Helena · Kisiwa cha Diego Garcia |
Categories: Mbegu | Fupi | Chad | Nchi za Afrika