Komori
From Wikipedia
|
|||||
Wito la taifa: Unité - Justice - Progrès (Umoja – Haki - Maendeleo) |
|||||
Wimbo wa taifa: Udzima wa ya Masiwa | |||||
Mji mkuu | Moroni |
||||
Mji mkubwa nchini | Moroni | ||||
Lugha rasmi | Shikomor, Kiarabu, Kifaransa | ||||
Serikali
Rais
|
Shirikisho la Jamhuri Azali Assoumani |
||||
Uhuru - tarehe |
kutoka Ufaransa 6 Julai 1975 pesa = Frank ya Komori |
||||
Eneo - Jumla - Maji (%) |
2,170 km² (ya 167) -- |
||||
Idadi ya watu - 2002 kadirio - Msongamano wa watu |
596,202 (ya 158) 275/km² (275) |
||||
Fedha | {{{currency}}} (KMF ) |
||||
Saa za eneo - Kiangazi (DST) |
(UTC+3) {{{time_zone_DST}}} (UTC{{{utc_offset_DST}}}) |
||||
Intaneti TLD | .km | ||||
Kodi ya simu | +269 |
Komori (pia: Visiwa vya Ngazija) ni nchi kwenye funguvisiwa na dola katika Bahari Hindi upande wa Mashariki ya Afrika. (Ki-komori: قمر Komori, kifaransa: Comores) Jina limetokana na lugha ya Kiarabu Juzur al-Qamar (جزر القمر) linamaanisha "visiwa vya mwezi"
- Pesa: 1 Frank ya Komori(FC)= 100 Centimes. 1€ = 491,9677 FC
- Sikukuu ya Taifa: 4. Julai
- Dini: 98 % Waislamu Wasunni, 2 % Wakatoliki
Contents |
[edit] Jiografia
Funguvisiwa ya Komori ina visiwa vitatu vikubwa: Grande Comore (Ngazidja), Anjouan (Nzwani) und Moheli (Mwali). Iko katika Kanali ya Msumbiji kaskazini ya Madagaska na mashariki ya Msumbiji. Kisiwa cha Mayotte ni sehemu ya funguvisiwa kijiografia lakini kisiasa sehemu ya Ufaransa kwa sababu wakati wa uhuru watu wa Mayotte walitamka kwa kura nyingi (73%) ya kwamba wanataka kukaa na Ufaransa.
Komori ni sehemu ya bara la Afrika. Ina pia visiwa mbalimbali vidogo. Hali ya hewa ni kitropiki. Kuna mvua miezi yote.
Kitovu cha kisiwa kikubwa Grande Comore ni mlima wa volkano hai Karthala mwenye 2461m. Safari iliyopita Karthala ililipuka mw. 1977 ikaharibu kijiji kimoja.
Miji mikubwa ni: (Wakazi wa hali ya 2005): Moroni 42.872, Mutsamudu 23.594, Fomboni 14.966, Domoni 14.509 na Tsémbehou 11.552.
[edit] Watu
Watu wa Komori ni mchanganyiko wa Waarabu, Wamadagaska, Waafrika wa bara ambao mababu walikuwa watumwa, Wahindi na Wazungu kadhaa. Kutokana na uhaba wa ajira Wakomori wengi wamehamia nje hasa Madagaska. Wakazi wengi ni Waislamu. Nusu ya watu wote hawajui kusoma.
[edit] Historia
[edit] Siasa
Kufuatana na katiba ya uhuru ya 1975 Komori ilitangazwa kuwa jamhuri ya Kiislamu. Serikali zilipinduliwa mara kwa mara na wanajeshi au na mamluki. Katiba mpya ya mwaka 2001 imeondoa tabia ya kidini ya dola na iliunda utaratibu wa urais kuzunguka kati ya visiwa vitatu vikubwa.
Katika muundo huo rais wa jamhuri atateuliwa kila baada ya miaka minne kutoka kisiwa tofauti. Katika uchaguzi ya mwaka 2002 rais Azali Assoumani alichaguliwa kutoka kisiwa cha Ngazidja (Komori Kuu). Katika uchaguzi wa 2006 rais amechaguliwa kati ya wagombea kutoka kisiwa cha Anjouan. Wananachi wa Anjouan walipiga kura ya kwanza. Wagombea watatu wenye kura nyingi wameteuliwa na kusimamishwa mbele ya wapiga kura wa visiwa vyote watakaomchagua rais wa jamhuri. Rais wa mwaka 2010 anatakiwa kutoka katika kisiwa cha Moheli, baadaye tena rais kutoka Ngazidja, n.k.
Katika uchaguzi wa 2006 ndiye Ahmed Abdallah Mohamed Sambi aliyepata kura nyingi kiasi cha 58% baada ya kempeni alipoahidi kupambana na ufisadi, kuwapatia wananchi ajira na kujenga nyumba kwa ajili ya maskini.
[edit] Uchumi
Komori ni kati ya nchi maskini zaidi duniani. Kilimo, uvuvi, uvindaji na misitu ni misingi ya uchumi wote. Barabara na mawasiliano ya meli au ndege ni haba, idadi ya watu inakua haraka, elimu ni duni; haya yote yanasababishi kudumu kwa uchumi wa kijungujiko na uhaba wa ajira. 80% ya wafanyakazi wote wanashughulika kilimo.
Nchi za Afrika | |
---|---|
Afrika ya Kati (Jamhuri ya) | Afrika Kusini | Algeria | Angola | Benin | Botswana | Burkina Faso | Burundi | Cabo Verde | Chad |Cote d'Ivoire | Djibouti | Eritrea | Gabon | Gambia | Ghana | Guinea | Guinea Bisau | Guinea ya Ikweta | Kamerun | Kenya | Komori | Kongo (Jamhuri ya) | Kongo (Jamhuri ya Kidemokrasia ya) | Lesoto | Liberia | Libya | Madagaska | Malawi | Mali | Misri | Morisi (Visiwa vya) | Mauritania | Moroko | Msumbiji | Namibia | Niger | Nigeria | Rwanda | Sahara ya Magharibi | Sao Tome na Principe | Senegal | Shelisheli | Sierra Leone | Somalia | Sudan | Tanzania | Togo | Tunisia | Uganda | Uhabeshi | Uswazi | Zambia | Zimbabwe | |
Maeneo ya kiafrika ambayo ni sehemu za nchi nje ya Afrika | |
Ufaransa: Mayotte · Réunion | Hispania: Visiwa vya Kanari · Ceuta · Melilla | Ureno: Visiwa vya Madeira | Uingereza: · Kisiwa cha St. Helena · Kisiwa cha Diego Garcia |
Makala hiyo kuhusu "Komori" bado ni mbegu. Unaweza kusaidia kuikuza kwa kubofya kitufe kilichoandikwa "hariri". Ikiwepo makala kuhusu Komori kwa lugha nyingine, unaweza kuitafsiri kwa Kiswahili. |