Msumbiji
From Wikipedia
|
|||
Lugha ya Taifa | Kireno | ||
Mji Mkuu | Maputo | ||
Aina ya Serikali | Jamhuri | ||
Rais | Armando Guebuza | ||
Waziri Mkuu | Luisa Diogo | ||
Eneo | 801.590 km² | ||
Wakazi | 19.406.703 (Julai 2005) | ||
Wakazi kwa km² | 24 | ||
JPT/ Mkazi | 233 US-$ (2004) | ||
Uhuru | kutoka Ureno tar. 25.06.1975 | ||
Pesa | Metical (MZM) | ||
Wakati | UTC +2h | ||
Wimbo ya Taifa | (inaangaliwa upya) | ||
Namba ya simu ya kimataifa | +258 | ||
Msumbiji (Kireno: Moçambique) ni nchi ya Afrika ya Kusini-Mashariki. Sikukuu ya Taifa ni tar. 25.06., kutokana na na uhuru mwaka 1975.
Msumbiji iko ufukoni wa Bahari Hindi ikipakana na Tanzania, Malawi, Zambia, Zimbabwe, Afrika Kusini na Uswazi. Upande wa mashariki kuna kisiwa cha Madagaska ng'ambo ya mlango bahari wa Msumbiji.
Jina la nchi imetokana na Kisiwa cha Msumbiji (kireno: Ilha de Moçambique) iliyokuwa boma na makao makuu ya Ureno kwenye pwani la Afrika ya Mashariki.
[edit] Jiografia
Tambarare ya pwani ni sehemu kubwa ya sehemu ya kusini ya nchi lakini kwenda kaskazini upana wake inapungua. Nyuma ya tambarare nchi inapanda hadi kufika uwiano wa tambarare ya juu ya Afrika ya Kusini. Milima mirefu zaidi inajulikana kama Inyanga yenye mita 2500 juu ya UB iko katika jimbo la Tete inayopakana na Zimbabwe, Zambia na Malawi.
Mito iko mingi ikiwa mkubwa ndio Zambezi, halafu Ruvuma mpakani na Tanzania, Save na Limpopo. Ziwa la Nyassa ni sehemu ya mpaka na Malawi.
Umbo la eneo la nchi ni ndefu sana ni kilomita 2000 kutoka mpaka na Tanzania upande wa Kaskazini hadi Maputo iliyoko karibu na Uswazi na Afrika Kusini. Pwani la Bahari Hindi ina urefu wa 2.470 km
Miji mikubwa zaidi ni Maputo (wakazi 1.191.613), Matola (wakazi 543.907) na Beira (wakazi 530.706).
[edit] Historia
Wakazi wa kwanza wa Msumbiji huaminiwa kuwa wavindaji Wasan. Katika karne za kwanza BK wahamiaji Wabantu walifika wenye ujuzi wa kilimo na uhunzi.
Haujulikani ni lini ya kwamba wafanyabiashara Waarabu walianza kufika ufukoni na kujenga vituo na miji yao. Lakini utamaduni wa Waswahili ulifika hadi sehemu za mwambao wa Msumbiji. Hadi leo aina ya Kiswahili inazungumzwa kwenye visiwa vya Kirimba.
Mto wa Zambezi ilitumika kama njia ya mawasiliano na biashara kati ya Ufalme wa Mwene Mtapa (Zimbabwe) na wafanyabiashara wa pwani.
Taarifa za kwanza ya kimaandishi zinaanza na kufika kwa Wareno. Mwaka 1498 Vasco da Gama alifika akiwa njiani kuelekea Bara Hindi.
Makala hiyo kuhusu "Msumbiji" bado ni mbegu. Unaweza kusaidia kuikuza kwa kubofya kitufe kilichoandikwa "hariri". Ikiwepo makala kuhusu Msumbiji kwa lugha nyingine, unaweza kuitafsiri kwa Kiswahili. |
Nchi za Afrika | |
---|---|
Afrika ya Kati (Jamhuri ya) | Afrika Kusini | Algeria | Angola | Benin | Botswana | Burkina Faso | Burundi | Cabo Verde | Chad |Cote d'Ivoire | Djibouti | Eritrea | Gabon | Gambia | Ghana | Guinea | Guinea Bisau | Guinea ya Ikweta | Kamerun | Kenya | Komori | Kongo (Jamhuri ya) | Kongo (Jamhuri ya Kidemokrasia ya) | Lesoto | Liberia | Libya | Madagaska | Malawi | Mali | Misri | Morisi (Visiwa vya) | Mauritania | Moroko | Msumbiji | Namibia | Niger | Nigeria | Rwanda | Sahara ya Magharibi | Sao Tome na Principe | Senegal | Shelisheli | Sierra Leone | Somalia | Sudan | Tanzania | Togo | Tunisia | Uganda | Uhabeshi | Uswazi | Zambia | Zimbabwe | |
Maeneo ya kiafrika ambayo ni sehemu za nchi nje ya Afrika | |
Ufaransa: Mayotte · Réunion | Hispania: Visiwa vya Kanari · Ceuta · Melilla | Ureno: Visiwa vya Madeira | Uingereza: · Kisiwa cha St. Helena · Kisiwa cha Diego Garcia |