Armenia
From Wikipedia
|
|||||
Wito la taifa: Kiarmenia: Մեկ Ազգ , Մեկ Մշակույթ "Mek Azg, Mek Mshakowyt" "Taifa moja, utamaduni moja" |
|||||
Wimbo wa taifa: Mer Hayrenik ("Nchi yetu") |
|||||
Mji mkuu | Yerevan1 |
||||
Mji mkubwa nchini | Yerevan | ||||
Lugha rasmi | Kiarmenia | ||||
Serikali | Jamhuri Robert Kocharian Andranik Margaryan |
||||
Uhuru Ilitangazwa Ilitambuliwa Ilikamilika chanzo cha taifa la Armenia kuanzishwa kwa ufalme wa Urartu kuanzishwa kwa ufalme wa Armenia kupokelewa kwa Ukristo Jamhuri ya Armenia |
23 Agosti 1990 21 Septemba 1991 25 Desemba 1991 11 Agosti 2492 KK 1000 KK 600 KK 301 28 Mei 1918 |
||||
Eneo - Jumla - Maji (%) |
29,800 km² (ya 141) 4.71 |
||||
Idadi ya watu - 2005 kadirio - 2001 sensa - Msongamano wa watu |
3,215,800[1] (ya 1362) 3,002,594 101/km² (ya 98) |
||||
Fedha | Dram (AMD ) |
||||
Saa za eneo - Kiangazi (DST) |
UTC (UTC+4) DST (UTC+5) |
||||
Intaneti TLD | .am | ||||
Kodi ya simu | +374 |
||||
1 Maandishi kwa herufi za Kilatini pia "Erevan", "Jerevan" au "Erivan". 2 cheo kulingana na kadirio ya UM ya 2005. |
Armenia (Kiarmenia: Հայաստան Hayastan au Հայք Hayq) ni nchi ya mpakani wa Ulaya na Asia katika milima ya Kaukasi iliyoko kati ya Bahari Nyeusi na Bahari ya Kaspi. Imepakana na Uturuki, Georgia, Azerbaijan na Iran. Upande wa kuisini ni eneo la nje la Kiazerbaijan linaloitwa Nakhichevan.
Mlima wa kitaifa wa armenia ni mlima Ararat unaoaminiwa ni mahali ambako safina ya Nuhu ilikuta nchi kavu baada ya mafuriko makubwa yanayosimuliwa katika Biblia.
Armenia ilikuwa sehemu ya Umoja wa Kisovyeti tangu 1920 ikapata uhuru wake tena 1991. Armeni ni kati ya mataifa ya kale kabisa duniani ingawa eneo lake limebadilika sana na eneo la kisasa ni sehemu ndogo tu ya maeneo yaliyokuwa ya Armenia katika karne na milenia za kale.
Armeni ilikuwa nchi ya kwanza ya kupokea Ukristo kama dini rasmi ya kitaifa mnamo mwaka 301. Ingawa kijiografia Armenia huhesabiwa mara nyingi kama sehemu ya Asia kiutamaduni na kihistoria huhesabiwa pia kama sehemu ya Ulaya.
Kuna fitina na nchi jirani ya Azerbaijan kuhusu eneo la Nagorno-Karabakh linalokaliwa na Waarmenia lakini ni sehemu ya Azerbaijan kisiasa. Mipaka hii ni urithi wa zamani za Umoja wa Kisovyeti. Palikuwa na vita kati ya nchi mbili. Hali halisi Armenia inatawala eneo hili ingawa Nagorno Karabakh ilijitangaza kuwa jamhuri ya kujitegemea isiyokubaliwa na umma wa kimataifa.
[edit] Viungo vya Nje
- Armenia.org - Complete history of Armenia, covering 800B.C. to 2004
- PanARMENIAN.Net - Daily Armenian News
Nchi na maeneo ya Asia |
Afghanistan | Armenia2 | Azerbaijan | Bahrain | Bangladesh | Bhutan | Brunei | China | Cyprus2 | Falme za Kiarabu | Georgia2 | Hong Kong3 | Indonesia | Iran | Iraq | Israel | Japan | Kambodia | Kazakhstan | Korea Kaskazini | Korea Kusini | Kuwait | Kirgizstan | Laos | Lebanon | Macau3 | Malaysia | Maldivi | Mongolia | Myanmar | Nepal | Oman | Pakistan | Palestina | Qatar | Urusi1 | Saudia | Singapore | Sri Lanka | Syria | Taiwan (Jamhuri ya China) | Tajikistan | Timor ya Mashariki | Ufilipino | Uthai | Uturuki1 | Turkmenistan | Uhindi | Uzbekistan | Vietnam | Yemen | Yordani |
1. Nchi ina maeneo katika Asia na Ulaya. 2. Nchi hii iko Asia lakini kwa sababu za kihistoria au kiutamaduni inahesabiwa pia kati ya nchi za Ulaya. 3. Eneo la pekee la China. |
Makala hiyo kuhusu "Armenia" bado ni mbegu. Unaweza kusaidia kuikuza kwa kubofya kitufe kilichoandikwa "hariri". Ikiwepo makala kuhusu Armenia kwa lugha nyingine, unaweza kuitafsiri kwa Kiswahili. |
Categories: Mbegu | Armenia | Nchi za Ulaya | Nchi za Asia | Kaukasi