Myanmar
From Wikipedia
|
|||||
Wito la taifa: | |||||
Wimbo wa taifa: Kaba Ma Kyei | |||||
Mji mkuu | Naypyidaw1 |
||||
Mji mkubwa nchini | Yangon | ||||
Lugha rasmi | Kiburma | ||||
Serikali
Mwenyekiti
Waziri Mkuu |
Halmashauri ya kijeshi Jenerali Than Shwe Soe Win |
||||
Uhuru Tarehe |
4 Januari 1948 | ||||
Eneo - Jumla - Maji (%) |
676,578 km² (ya 40) 3.06% |
||||
Idadi ya watu - July 2005 kadirio - 1983 sensa - Msongamano wa watu |
50,519,0002 (ya 24) 33,234,000 75/km² (ya 119) |
||||
Fedha | Kyat ya Myanmar (K) (mmK ) |
||||
Saa za eneo - Kiangazi (DST) |
MMT (UTC+6:30) {{{time_zone_DST}}} (UTC{{{utc_offset_DST}}}) |
||||
Intaneti TLD | .mm | ||||
Kodi ya simu | +95 |
||||
1Serikali kadhaa hutambui Yangon kama mji mkuu. |
Myanmar (pia: Myama; Myamari) ni nchi ya Asia ya Kusini-Mashariki inayojulikana pia kwa jina la Burma au Bama. Imepakana na China upande wa kaskazini, Laos upande wa mashariki, Uthai kwa kusini-mashariki, Bangladesh na Uhindi. Kuna pwani la Bahari Hindi lenye urefu wa 2,000 km.
Contents |
[edit] Jiografia
Kaskazini ya nchi ina milima mingi. Safu tatu za Rakhine Yoma, Bago Yoma na Nyanda za Juu za Shan zimeanza katika Himalaya na kuelekea kusini. Milima ya Hengduan Shan iko mpakani na China. Mlima mkubwa ni Hkakabo Razi kwenye jimbo la Kachin mwenye kimo cha 5,881 m.
Mito mitatu mikubwa ya Myanmar inavuka kati ya safu za milima ni
- Ayeyerwady
- Thanlwin
- Sittang
Mto Ayeyarwady ni mto mkubwa wa Myanmar mwenye urefu wa 2,170 km. Bonde lake ni ya rutba lina wakazi wengi.
Karibu nusu ya nchi ni misitu.
[edit] Utamaduni
Myanmar ni nchi ya makabila mengi na lugha nyingi. Wakazi walio wengi hufuata dini ya Ubuddha. Kundi kubwa ni Waburma wenye asili katika milima ya Tibet walikotoka mababu yao miaka 1000 iliyopita.
[edit] Historia
Tangu karne ya 9 BK nchi iliona falme mbalimbali zilizotawala kutoka mji mkuu wa Pagan. Katika karne ya 19 Uingereza ulianza kujishughulisha na habari za Burma (Myanmar) baada ya kutawala maeneo jirani ya Uhindi. Kwa vita tatu kati ya 1826 na 1885 Uingereza ulieneza utawala wake. Burma ilikuwa sehemu ya Uhindi wa Kiingereza tangu 1885. 1937 Waingereza walianza kutawala Burma kama koloni ya pekee.
Wakati wa Vita Kuu ya Pili ya Dunia Japon ilitwaa karibu nchi yote. Baada ya vita Burma ikapata uhuru wake 4 Januari 1948.
Serikali iliyochaguliwa kidemokrasia ilipinduliwa 1962 kwa mapinduzi ya kijeshi. Mtawala mpya alikuwa jenerali Ne Win hadi 1988 aliyetangaza siasa ya "Ujamaa wa Kiburma". Upinzani ulikandamizwa mara kadhaa vikali.
Nchi iliona harakati kwa ajili ya demokrasia na dhidi ya udikteta mwaka 1988. Ne Win alijiuzulu. Baada ya maandamano yaliyokandamizwa mara kadhaa Jenerali Saw Maung alichukua utawala kwa nguvu ya kijeshi. Uchaguzi huru wa 1989 ilileta ushindi wa chama cha NLD, chini ya Aung San Suu Kyi. lakini kamati ya kijeshi ilikataa kukabishi serikali.
Burma ilibadilishwa jina kuitwa "Myanmar" ikaendelea kutawaliwa na serikali ya kijeshi. Upinzani hauruhusiwi.
[edit] Picha
Nchi na maeneo ya Asia |
Afghanistan | Armenia2 | Azerbaijan | Bahrain | Bangladesh | Bhutan | Brunei | China | Cyprus2 | Falme za Kiarabu | Georgia2 | Hong Kong3 | Indonesia | Iran | Iraq | Israel | Japan | Kambodia | Kazakhstan | Korea Kaskazini | Korea Kusini | Kuwait | Kirgizstan | Laos | Lebanon | Macau3 | Malaysia | Maldivi | Mongolia | Myanmar | Nepal | Oman | Pakistan | Palestina | Qatar | Urusi1 | Saudia | Singapore | Sri Lanka | Syria | Taiwan (Jamhuri ya China) | Tajikistan | Timor ya Mashariki | Ufilipino | Uthai | Uturuki1 | Turkmenistan | Uhindi | Uzbekistan | Vietnam | Yemen | Yordani |
1. Nchi ina maeneo katika Asia na Ulaya. 2. Nchi hii iko Asia lakini kwa sababu za kihistoria au kiutamaduni inahesabiwa pia kati ya nchi za Ulaya. 3. Eneo la pekee la China. |
Makala hiyo kuhusu "Myanmar" bado ni mbegu. Unaweza kusaidia kuikuza kwa kubofya kitufe kilichoandikwa "hariri". Ikiwepo makala kuhusu Myanmar kwa lugha nyingine, unaweza kuitafsiri kwa Kiswahili. |