Morisi
From Wikipedia
|
|||||
Wito la taifa: Stella Clavisque Maris Indici (Kilatini: Nyota na ufunguo wa Bahari Hindi) |
|||||
Wimbo wa taifa: Taifa | |||||
Mji mkuu | Port Louis |
||||
Mji mkubwa nchini | Port Louis | ||||
Lugha rasmi | Kiingereza, Kifaransa | ||||
Serikali
Rais
Waziri Mkuu |
Jamhuri Anerood Jugnauth Navinchandra Ramgoolam |
||||
Uhuru kutoka Uingereza |
12.03.1968 | ||||
Eneo - Jumla - Maji (%) |
2,040 km² (ya 169) 0.05 |
||||
Idadi ya watu - Julai 2005 kadirio - Msongamano wa watu |
1,230,602 (ya 155) 603/km² (ya 11) |
||||
Fedha | Mauritian Rupee (MUR ) |
||||
Saa za eneo - Kiangazi (DST) |
(UTC+4) (UTC) |
||||
Intaneti TLD | .mu | ||||
Kodi ya simu | +230 |
Morisi inaitwa rasmi "Jamhuri ya Morisi" (Kiingereza: Republic of Mauritius, Kifaransa: République de Maurice) ni nchi ya visiwa katika Bahari Hindi takriban 900 km mashariki ya Madagaska na 4000 km kusini-magharibi ya Bara Hindi. Eneo la jamhuri ni pamoja na kisiwa cha Morisi yenyewe, kisiwa cha Rodrigues, visiwa vidgo vya Cargados Carajos na Agalega. Hivi vyote ni sehemu ya funguvisiwa ya Maskarena pamoja na kisiwa cha kifaransa cha Réunion. Mji Mkuu wa jamhuri ni Port Louis.
[edit] Eneo la Jamhuri ya Morisi
Visiwa vya jamhuri vimesambaa katika eneo pana sana:
Kisiwa kikuu cha Morisi ni 1865km² au 91 % za ardhi yote ya jamhuri. Karibu wote wa wakazi milioni 1.2 huishi hapo.
Kisiwa cha Rodrigues kipo 560 km mashariki ya Morisi yenyewe. Eneo lake ni 109 km² kuna wakazi 40.000.
Visiwa vya Cargados Carajos (vianitwa pia Saint Brandon) ni visiwa 16 vidogo sana vyenye eneo la 1.3 km² pekee. Viko 300 km kaskazini ya Morosi.Kuna wakazi wachache wavuvi
Agalega ni visiwa viwili yaani Kisiwa cha Kaskazini na Kisiwa cha Kusini takriban 1,122 Km kaskazini ya Morisi yenyewe. Visiwa vina eneo la 70 km². Kuna vijiji vya Vingt Cinq na La Fourche kwenye kisiwa ha kaskazini na kijiji cha Ste Rita kwenye kisiwa cha kusini. Wenyeji wanalima mazao ya mnazi pamoja na mboga wa matumizi wao wenyewe.
[edit] Wakazi
Watu wa Morisi ni mchanganyiko kutokana na historia ya visiwa hivi. Wakazi wa kwanza walikuwa Waholanzi hawakuacha dalili isipokuwa majina ya mahali kwa sababu waliacha visiwa na kuondoka mwaka 1710 baada ya kushindwa kiuchumi.
Wafaransa walitawala visiwa kati ya 1715 hadi 1810. Walianzisha miji na mashamba ya miwa. Nje ya walowezi Wafaransa walipeka pia watumwa kutoka Afrika. Mwaka 1767 walikuwepo Wafaransa 3,163 pamoja na watumwa Waafrika 15,000 pia Wahindi 587.
Uingereza ulichukua utawala wa visiwa mwaka 1810 katika vita dhidi ya Napoleon. Tangu siku zile Kiingereza kilikuwa lugha rasmi ya serikali lakini wakazi waliendelea kutumia lahaja ya Kifaransa. Baada ya kuwapatia watumwa uhuru Waingereza walileta Wahindi wengi baadaye pia Wachina kama wafanyakazi kwenye mashamba ya sukari. Leo hii idadi kubwa ya wakazi ni wa asili ya Kihindi.
Lakini 80% ya wananchi hutumia aina ya Kifaransa kama lugha ya kwanza. Asilimia 15 hutumia lugha za Kihindi, wengine Kichina na Kiingereza.
Karibu nusu ya wakazi hufuata dini ya Uhindu, 35% Ukristo (hasa Wakatoliki), 12% ni Waislamu Wasunni, 3% Washia, 1% Wabuddha.
[edit] Uchumi
Hadi leo kilimo cha miwa (sukari) ni mgongo wa uti wa uchumi wa Morisi. Nchi iliendelea na serikali zilizochaguliwa bila kupinduliwa na hali hii ya utulivu ilisaidia kukua kwa uchumi. Hali ya maisha ni juu kuliko nchi nyingi za Afrika.
Makala hiyo kuhusu "Morisi" bado ni mbegu. Unaweza kusaidia kuikuza kwa kubofya kitufe kilichoandikwa "hariri". Ikiwepo makala kuhusu Morisi kwa lugha nyingine, unaweza kuitafsiri kwa Kiswahili. |
Nchi za Afrika | |
---|---|
Afrika ya Kati (Jamhuri ya) | Afrika Kusini | Algeria | Angola | Benin | Botswana | Burkina Faso | Burundi | Cabo Verde | Chad |Cote d'Ivoire | Djibouti | Eritrea | Gabon | Gambia | Ghana | Guinea | Guinea Bisau | Guinea ya Ikweta | Kamerun | Kenya | Komori | Kongo (Jamhuri ya) | Kongo (Jamhuri ya Kidemokrasia ya) | Lesoto | Liberia | Libya | Madagaska | Malawi | Mali | Misri | Morisi (Visiwa vya) | Mauritania | Moroko | Msumbiji | Namibia | Niger | Nigeria | Rwanda | Sahara ya Magharibi | Sao Tome na Principe | Senegal | Shelisheli | Sierra Leone | Somalia | Sudan | Tanzania | Togo | Tunisia | Uganda | Uhabeshi | Uswazi | Zambia | Zimbabwe | |
Maeneo ya kiafrika ambayo ni sehemu za nchi nje ya Afrika | |
Ufaransa: Mayotte · Réunion | Hispania: Visiwa vya Kanari · Ceuta · Melilla | Ureno: Visiwa vya Madeira | Uingereza: · Kisiwa cha St. Helena · Kisiwa cha Diego Garcia |